Advertisements

Wednesday, April 24, 2024

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA ATUNUKIWA NA RAIS NISHANI YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANZANIA, LEO IKULU CHAMWINO, DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemvalisha nishani ya Kumbukumbu ya miaka 60 ya Muungano Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Mzee Ramadhani Nyamka leo Aprili 24, 2024 Ikulu chamwino Jijini Dodoma

SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZA FEDHA ZA KUTOA MIKOPO KUFUATA UTARATIBU


Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mbunge Viti Maalum aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa Taasisi za Fedha zinatoa mikopo yenye riba kubwa kinyume na muongozo wa BoT.

Na. Josephine Majura, WF, Dodoma
Serikali imesema kuwa inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kisera, kiutawala na kisheria ili kudhibiti tabia ya baadhi ya taasisi za fedha kutoa mikopo kinyume na miongozo iliyopo.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mbunge Viti Maalum aliyetaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali kwa Taasisi za Fedha zinatoa mikopo yenye riba kubwa kinyume na muongozo wa BoT.

Mhe Chande, alisema kuwa Serikali imekuwa ikiendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Fedha inayolenga kusimamia ukwasi katika mfumo wa kibenki ili kuendana na mahitaji halisi ya kiuchumi na kuweka mazingira rafiki ya utoaji mikopo.

“Serikali imekuwa ikiendelea kuhimiza benki kuwasilisha taarifa za wakopaji pamoja na kutumia kanzidata ya taarifa za wakopaji (credit reference bureau) wakati wa uchambuzi wa maombi ya mikopo ili kupunguza vihatarishi vya ongezeko la mikopo chechefu”, alisema Mhe. Chande.

WATUMISHI WIZARA YA FEDHA WATAKIWA KUENDELEA KUZINGATIA SHERIA


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El - Maamry Mwamba, akizungumza kuhusu watumishi kuendelea kufuata Sheria na Misingi ya Utawala Bora, wakati akifungua mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi.Jenifa Omolo akiwataka watumishi wa Wizara kutoa maoni yao yatakayosaidia katika kuboresha utendaji wakati wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bi. Jenifa Omolo, Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali, Bw. Benjamin Magai na Naibu Katibu Mkuu TUGHE Taifa Bw. Regemalila Rutatina. Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Fedha Bi. Scholastica Okudo, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Bw. Tumwesige Kazura, Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Leonard Mkude
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano wa 37 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha, wakifuatilia mawasilisho mbalimbali wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU, CCM AWAPONGEZA MABALOZI WAKIKAMILISHA WARSHA YA SIKU 4 KIBAHA


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Mabalozi wa Tanzania wanaoshiriki warsha ya siku 4 katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha, Pwani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akizungumza wakati akiongoza warsha ya siku 4 ya Mabalozi iliyofanyika katika Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere mjini Kibaha, Pwani.

UMEME KWENYE GRIDI YA TAIFA WAFIKIA MEGAWATI 2,138


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb)wakati akiwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 katika Mkutano wa Kumi na Tano Kikao cha Kumi na Tatu.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko (Mb), ameliambia bunge kuwa katika mwaka 2023/2024 kuwezo wa mitambo ya kufua umeme iliyounganishwa kwenye mfumo wa Gridi ya Taifa umepanda kutoka Megawati (MW) 1,872.1 na kufikia Megawati (MW) 2,138, sawa na ongezeko la asilimia 14.2%.

Mhe. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Aprili 24, 2024 wakati akiwasilisha bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 katika Mkutano wa Kumi na Tano Kikao cha Kumi na Tatu.

RAIS WA ZANZIBAR DKT. MWINYI AFUNGUA JENGO LA SKULI YA SEKONDARI YA KIWANI PEMBA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na (kushoto) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein wakiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari Kiwani Wilaya ya Mkoani Pemba, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya sherehe za Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi na Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, wakisome maelezo ya Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Kiwani, baada ya kukamilika ujenzi wake, ikiwa shamrashamra za sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tannganyika na Zanzibar,ufunguzi huo iliofanyika  23-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Skuli ya Sekondari Kiwani Wilaya ya Mkoani Pemba na (kushoto kwa Rais) Mke wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Mattar Zahor Masoud, wakati wa shamrashamra za sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Muonekano wa Jengo Jipya la Skuli ya Sekondari Kiwani lililojengwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na kufunguliwa leo 23-4-2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALIMBALI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tatu Mhe. Fredrick kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mohamed Gharib Bilal kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku na kumvalisha Nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Samwel Malecela kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mama Janeth Magufuli Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo aliipokea kwa niaba ya Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Aprili, 2024. Nishani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hutunukiwa kwa Wakuu wa Nchi Wastaafu (hai au marehemu) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioingia madarakani kwa njia ya kikatiba na wameendelea kuonesha Maadili mema yenye nidhamu, heshima na mfano wa kuigwa.

WAKUU WA WILAYA TATU ZA MKOA WA KILIMANJARO WAKABIDHIWA MAGARI MAPYA


Na WILLIUM PAUL, MOSHI.
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amekabidhi magari matatu kwa ajili ya wakuu wa wilaya za Rombo, Mwanga na Same ili kuongeza ufanisi wa utendaji na kuleta maendeleo ya mkoa yenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano hayo nje ya viwanja wa ofisi za mkuu wa mkoa, Babu amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanza kutekeleza maombi mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro ya kuwapatia Wakuu wa wilaya vitendea kazi.

Babu alisema kuwa, Wabunge wamekuwa wakilalamika Bungeni kuhusiana na wakuu wa wilaya kukosa magari ambapo mkoa ulipanga kuhakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu wawe wameshanunua magari matatu ya wakuu wa wilaya.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa, magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za kiserikali na kuwataka kwenda kuyatunza magari hayo kwani yamenunuliwa kwa gharama.

MBUNGE MTATURU ACHANGIA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA ELIMU



JITIHADA za Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu kwa kushirikiana na wanachi zimesaidia kukamilisha kazi ya upauaji wa madarasa mawili katika Shule Shikizi ya Mwitumi hatua itakayoondoa changamoto ya watoto kusafiri umbali wa kilomita 9 na kuvuka mito miwili kufuata shule mama ya Msingi Nkundi.

Katika jitihada hizo wananchi walitumia nguvu yao kujenga hadi usawa wa Lenta na mbunge akawaunga mkono kwa kutoa Sh Milioni 13 ambazo zilinunua Bati 110, mbao zote na Saruji ya kupiga lipu na Sakafu.

Akizungumza na kituo hiki April 24,2024,Mtaturu amesema kukosekana kwa madarasa hayo kumesababisha utoro wa wanafunzi wakati wa masika na hivyo kushusha kiwango cha ufaulu.

Amewashukuru wananchi wa Kitongoji cha Mwitumi, Kijiji cha Nkundi Kata ya Kikio kwa Ushirikiano mkubwa walioutoa wa kushirikiana nae na kumaliza shughuli ya ujenzi wa Darasa

RAIS DKT. MWINYI AZINDUA MRADI WA BARABARA PEMBA




RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Mradi wa Barabara Maeneo Huru ya Uchumi Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, mradi huo uliozinduliwa leo 23-4-2024,ikiwa ni shamrashara za sherehe za Maadhimisho ya Miako 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mkurugenzi wa ZIPA Pemba na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara maeneo huru ya Uchumi Micheweni Mhandisi Suleiman Abdallah Ali akitowa maelezo ya Mradi huo wakati wa Uzinduzi wa wa Barabara ya Maeneo Huru ya Uchumi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni shamrashara za sherehe za Maadhimisho ya Miako 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,uzinduzi huo uliofanyika leo 23-4-2024 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe.Shariff Ali Shariff

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Barabara ya Maeneo Huru ya Uchumi Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni Shamrashamra za sherehe za Maadhimisho ya Miako 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mbarouk Khatib na (kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mhe.Shariff Ali Shariff na Mkurugenzi wa IRIS Mr.Suleiman,uzinduzi huo uliofanyika leo 23-4-2024


WIZARA YA FEDHA NA NA EAC WAJADILI UKUSANYAJI MAPATO YA NDANI KWA AJILI YA MAENDELEO



Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza katika mkutano uliotishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF na kuwakutanisha Wadau kutoka nchi za Afrika Mashariki, wakati wa mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings), jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo walijadili namna nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoweza kujitegemea kwa kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani badala ya kutemea mikopo na misaada kutoka nje.
Mkutano ulioitishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF ukiendelea, wakati wa mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings), jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo wadau walijadili namna nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoweza kujitegemea kwa kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani badala ya kutemea mikopo na misaada kutoka nje.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, wakifuatilia mkutano uliotishwa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, wakati wa mikutano ya Kipupwe (Spring Meetings), jijini Washington D.C nchini Marekani, ambapo wadau walijadili namna Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinavyoweza kujitegemea kwa kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani badala ya kutemea mikopo na misaada kutoka nje.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF,Washington)

Tuesday, April 23, 2024

PSPTB YATOA ELIMU CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR

 

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Godfred Mbanyi akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Afisa TEHAMA kutoka PSPTB Elihuruma Eliufoo akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili pamoja na kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Afisa Ununuzi kutoka Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), AllyYassin Mbarouk akitoa maelezo kuhusu namna ya kuongeza dhamani kwenye taaluma hiyo kwa wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

DKT. DIMWA : AJIVUNIA HAZINA YA WAZEE WA CCM


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na kada wa CCM ndugu Waalidi Psinarie Kavishe(wa kwanza kushoto) nyumbani kwake Kwa mchina mwanzo Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa(upande wa kulia),akizungumza na Kadhi Mkuu mstaafu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis nyumbani kwake Mwanakwerekwe Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba mstaafu ndugu Salum Juma Tindwa nyumbani kwake kwa Mchina Unguja.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, akizungumza na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Wanawake na Watoto Zanzibar ndugu Msham Abdallah Khamis nyumbani kwake Chuini Unguja.

ZANZIBAR YAUNGANA NA DUNIA KUADHIMISHA KILELE CHA WIKI YA MAABARA DUNIANI


Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akikata utepe kuashiria uzinduzi wa sera ya maabara Zanzibar katika kilele cha wiki ya maabara iliyofanyika ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa ndege Zanzibar.

Na Fauzia Mussa, Maelezo
Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wataalamu wa Maabara kuvifanyia utafiti vitu wanavyovichunguza ikiwemo maradhi ili kuyadhibiti kwa njia za kisayansi.

Akisoma hotuba ya Rais Mwinyi katika kilele cha wiki ya Maabara Duniani huko Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar alipomwakilisha, Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema kufanya hivyo kutasaidia taasisi kudhibiti maradhi na kuzielekeza njia zinazoshauriwa kirahisi kutokana na kuwepo na ushahidi wa Kisayansi.

Aidha amewataka wataalamu hao kuongeza nguvu kwenye Taasisi za Tafiti ikiwemo za Taaisi ya Afya ya Binaadamu (ZAHRI), Utafiti wa Mifugo (ZALIRI), Taasisi ya Utafiti wa Safayansi ya Baharini (ZAFIRI) ili kuweza kufikia malengo yaliokusudiwa.

Amefahamisha kuwa Maabara zote zina mchango mkubwa kwa maendeleo mbalimbali ikiwemo ya afya na huduma zinazotolewa kwa wananchi, hivyo Serikali itaendelea kuimarisha Maabara zote ili kuweza kuendeleza kazi za uchunguzi wa maradhi, vinasaba, kemikali, pamoja na vyakula.

RAIS WA DK.HUSSEIN MWINYI AMEJUMUIKA NA WANAVYUONI NA MASHEIKH KATIKA HAULI NA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU ALHABYB AHMAD BIN ABUUBKAR SUMEIT



RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kumuombea marehemu Mwanachuoni Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit ikisomwa na Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein (kushoto kwa Rais) wakiwa katika kaburi la marehemu lililoko katika eneo la Msikiti wa Ijumaa Malindi Wilaya Mjini Unguja, wakati wa hafla ya Hauli ya 102 iliyofanyika leo 22-4-2024 na (kushoto kwake) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Masheikh na Wananchi mbalimbali katika Kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombe Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe.Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Sheikh. Sayy Mudh-hiridin Ally Qullatein


SAYY.Omar Bin Ally Qullatein akihitimisha kisomo cha Hauli ya 102 ya kumuombea Marehemu Mwanachuoni Mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit, iliyofanyika leo 22-4-2024 katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Malindi Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, na (kushoto kwake) Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume

Sunday, April 21, 2024

WAZIRI MKUU AWAAGA VIONGOZI WA DINI, UZINDUZI WA ROUTE YA SGR DAR - DODOMA

L
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaaga viongozi wa dini 104 ambao wanaelekea Dodoma kwa treni ya mwendokasi (SGR) kwenda kushiriki ibada maalum ya kuliombea Taifa inayotarajiwa kufanyika kesho, Jumatatu, Aprili 22, 2024.

Treni hiyo imeondoka stesheni ya Dar es Salaam saa 8.53 mchana ikiwa na viongozi hao, waandishi wa habari, waimbaji wa nyimbo za injili na kaswida, viongozi wastaafu wa Serikali, watendaji wa Shirika la Reli nchini, wawakilishi wa ubalozi na watedaji wengine wa Serikali.
Amewaaga viongozi hao na watendaji wengine wa Serikali na taasisi mbalimbali leo (Jumapili, Aprili 21, 2024) kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye stesheni ya Tanzanite, barabara ya Sokoine, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na viongozi hao kabla ya kupata dua ya kuombea safari yao, Waziri Mkuu amesema: “Leo ni siku muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Tuko kwenye wiki ya maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano na tunashuhudia safari ya kwanza ya treni ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.”