Advertisements

Tuesday, December 6, 2016

Waziri Nape afunga Mkutano Mkuu wa Waandishi wa habari za Mitandao 'Tanzania Bloggers Network' (TBN),ahidi kuanzisha tuzo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa Ufafanuzi wakati alipokuwa akieleza namna ya kuitambua mitandao ya Kijamii pamoja na uanzishaji wa Tuzo kwa Waendeshaji mitandao hiyo.
Waziri Nape alisema kuwa lengo la tuzo hizo ni kuzisaidia blogs za Tanzania kubobea katika nyanja tofauti ikiwemo kilimo, mifugo, viwanda, hifadhi ya jamii kwa nia ya kuipa heshima tasnia ya habari nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza mapema leo jijini Dar wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Tanzania Bloggers Network (TBN) iliokwenda sambamba na semina ya wanachama wa umoja wa waendeshaji wa blog nchini.Picha na Michuzi Jr.

DICOTA: 2016 National Land Policy Stateholders' Feedback.


The Diaspora Council of Tanzania (DICOTA) is pleased to release the feedback of  2016 Tanzania National Land Policy. The document reflects the many comments DICOTA received and, results  of the proposed land policy  interpretation. We would like to take this opportunity  to express our appreciation to all who responded to the call to action and provided feedback.

To read the synthesis go here: http://dicotaus.org/2016-land-policy-stakeholders-input/
:

UMEME WA UPEPO KUINGIZWA KWENYE GRIDI YA TAIFA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuingiza umeme wa upepe kwenye grid ya taifa mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau mbalimbali wa umeme.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki imesema iko kwenye mchakato wa kuingiza umeme huo kwenye gridi ya taifa, baada ya kukidhi vigezo vya kitaifa.
Akizungumza leo Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte alisema mradi huo unafanywa kwa ushirikiano na taasisi ya fedha ya Kimataifa iliyochini ya benki ya dunia.

WAZIRI MKUU AKITEMBELEA MRADI WA UMWAGILIAJI KARATU

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau, mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la World Vision.wakwanza kulia ni Mkurugenzi wa Miradi katika shirika hilo Revocatus Kamara.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea Mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Jobag wilaya ya Karau ,mradi uliojengwa kwa ufadhili wa shirika la World Vision.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, KATIBU MKUU PAMOJA NA NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza mpaka hapo mamlaka husika itakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.


Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo leo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.


"Kumeibuka tabia ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuwafukuza Wamachinga bila utaratibu wowote wa wapi wanawapeleka na wakati mwingine wanapelekwa maeneo ya mbali ambayo hayafai hata kwa kufanya biashara, hili jambo sio sawa hata kidogo.


"Sipendi Wamachinga wafanye biashara kwenye hifadhi ya barabara lakini hakuna sheria katika nchi hii inayosema mtu wa biashara ndogondogo au Mmachinga hatakiwi kukaa katikati ya mji, tukianza kwenda kwenye utaratibu wa namna hiyo maana yake tunaanza kutengeneza  madaraja ya Watanzania, kwamba kuna Watanzania fulani wa daraja fulani wanapaswa kukaa katikati ya mji na Watanzania wa daraja fulani hawatakiwi kukaa katikati ya mji, huo sio mwelekeo wetu na wala Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo mimi na wewe (Makamu wa Rais) tulipita kuinadi, haisemi tutengeneze madaraja ya watu wanaostahili kukaa mjini na wengine hawastahili kukaa mjini, sasa nimeona hili nilizungumze na nataka kulirudia kwa mara ya mwisho" amesema Rais Magufuli.


Dkt. Magufuli ameelekeza kuwa Wamachinga waliondolewa katika maeneo yao Jijini Mwanza waachwe waendelee na shughuli zao mpaka hapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza itakapokamilisha maandalizi ya mahali watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha Wamachinga wenyewe.

HEAD, INC ANNUAL GALA DINNER BEST MOMENTS

INC annual dinner iliyofanyika siku ya Jumamosi Dec 3, 2016  Hamton Inn Cpllege Park Maryland na kuhudhuriwa na wakazi wa DMV na vitongoji vyake
INC gala dinner iliyofanyika siku ya Jumamosi Dec 3, 2016 Hampton Inn College Park Maryland,
INC annual dinner iliyofanyika siku ya Jumamosi Dec 3, 2016  Hamton Inn Cpllege Park Maryland na kuhudhuriwa na wakazi wa DMV na vitongoji vyake
INC gala dinner iliyofanyika siku ya Jumamosi Dec 3, 2016 Hampton Inn College Park Maryland,
 
INC annual dinner iliyofanyika siku ya Jumamosi Dec 3, 2016  Hamton Inn Cpllege Park Maryland na kuhudhuriwa na wakazi wa DMV na vitongoji vyake

TOZOLA, Book Now, Pay LaterTANZANIA ASSOCIATION IN OREGON


Michigan Tanzania Independence Party

TANZANIA UHURU NIGHT COLUMBUS, OHIO


NUNUA TIKETI MAPEMA KWA NUSU BEI MWISHO NI NOVEMBA 30,2016

Serikali ya Tanzania na Mauritius kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Sanaa na na Utamaduni.

 Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa,na Michezo Mhe. Anastazia Wambura(wa pili kulia) akizungumza na Ujumbe  wa Serikali ya Mauritius pamoja na  baadhi ya viongozi wa Wizara  leo Jijini Dar es Salaam  alipokutana na Waziri wa Sanaa na Utamaduni Mhe. Santaram Baboo (wa kwanza kulia) kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya Sanaa na Utamaduni.Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo  wakiwa katika mazungumzo na Uongozi wa Mauritius kuhusu kuimarisha sekta ya Sanaa na Utamaduni leo Jijini Dar es Salaam.

MAGEREZA YAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa(wa pili kulia) akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna Gaston Sanga(wa kwanza kushoto) ni Afisa Uhusiano wa Kampuni ya SAN LAM, Bw. Rishia Kileo. Vifaa hivyo vitatumiwa na Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza katika Mashindano ya Kijeshi yanayotarajiwa kufanyika Zanzibar mwezi huu Desemba, 2016.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Dkt. Juma Malewa akitoa neno la shukrani kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vilivyotolewa na Kampuni ya SAN LAM Life Insurance. Hafla hiyo imefanyika leo Desemba 06, 2016 katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Kamishna wa Magereza Gaston Sanga(kulia) ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni SAN LAM Life Insurance, Bw. Samuel Mika.

SALAMU ZA RAMBI RAMBI - KIFO CHA PROF. MTULIA

Image result for chama cha mapinduzi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg. Mwishehe Shaban Mlao kufuatia kifo cha Profesa Idrissa Ali Mtulia, Mbunge mstaafu wa Jimbo la Rufiji kilichotokea jana tarehe 05 Desemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Prof Mtulia ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi na utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Katibu Mkuu wizara mbalimbali, Daktari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili na Mwenyekiti wa Bodi ya Madawa (MSD)

Prof Mtulia, atakumbukwa na wanachama wa CCM na Wananchi wa Mkoa wa Pwani kwa jitihada zake za ujenzi na uimarishaji wa Chama na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Wananchi wa Rufiji.

Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 

Imetolewa na:-
                   
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
06.12.2016

SERIKALI YATAKIWA KUBAINISHA STENDI ZA DALADALA JIJINI MWANZA

 Mwenyekiti wa Madereva Kanda ya ziwa Hassan Dede akihojiwa na waandishi wa habari
Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa wamezisimamisha Daladala kwa kosa la kupakia abira eneo ambalo sio rasmi

MATUKIO YA UHAKIKI WA WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA MKOANI ARUSHA

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto)  akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango namna zoezi zima la uhakiki wa wastaafu kanda ya kaskazini linavyokwenda kabla ya uzinduzi wa zoezi hilo. Zoezi hili ni kwa mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga. 
Zoezi la kuhakiki wastaafu likiendelea katika Ofisi za Makao Makuu, Halmashauri ya jiji la Arusha, Pichani ni baadhi ya wastaafu wakifanyiwa uhakiki.

MAITI INAYOGOMBEWA SASA KUZIKWA DAR

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru mwili wa marehemu Ernest Materego uliosafirishwa Novemba 24, mwaka huu kwenda Bunda kwa maziko urejeshwe na kuzikwa Dar es Salaam.

Hukumu hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi tisa wa pande mbili zilizokuwa zikibishaniwa wapi marehemu azikwe.

Materego alifariki Novemba 19, mwaka huu jijini Dar es Salaam na Novemba 24 mdogo wa marehemu, Gonche Materego aliyekuwa akimuuguza na wenzake walisafirisha mwili huo kwa ajili ya mazishi Bunda mkoani Mara.

Watoto wa marehemu, Joyce, Edwin, Rita, Irene na mama yao mzazi, Dinah Willige (65) walipinga mahakamani wakiomba mwili urejeshwe wazike Dar es Salaam kwa sababu wanadai baba yao aliwaambia akifariki azikwe Dar es Salaam.

Wadaiwa akiwamo mdogo wa marehemu, Gonche, mke mdogo wa marehemu, Mwajuma Hassani (39), rafiki wa marehemu Thobias Mwita (66) pamoja na  majirani walitaka mwili huo uzikwe Bunda wakidai kuwa marehemu alitaka kuzikwa kwao.

CUF Wakanusha Taarifa za Maalim Seif Kutaka Kukihama Chama Hicho

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwamba Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad anataka kuhama chama hicho ni za kupuuzwa kwa kuwa hazina ukweli.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema hayo jana  baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Maalim anataka kuondoka ndani ya chama hicho cha upinzani.

Alisema tangu kuibuka kwa mgogoro ndani ya CUF na Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba imekuwapo mikakati ya kuwakatisha tamaa jambo ambalo halitafanikiwa.

Mazrui alisema wanaopanga mikakati wamehangaika kila njia na wameonekana kukwama, hivyo kuibuka na mkakati wa kumzushia Katibu Mkuu kuhama chama.

AJALI YA LORI NA HIACE YAUA WATU 9 NA KUJERUHI 18

Watu tisa wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Ifunda mkoani Iringa jana baada ya lori kugonga gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace. 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alisema dereva wa lori hilo lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Dar es Salaam, alishindwa kufunga breki na kuigonga Hiace hiyo iliyokuwa imeegeshwa pembeni ya barabara. 

MAGAZETI YA LEO DESEMBA 06, 2016

Monday, December 5, 2016

Kijana Mzalendo atoa sababu za kufungwa kiwanda cha Dangote

SHEREHE ZA MIAKA 55 YA UHURU WA MTANZANIA KATIKA JIJI LA WAJANJA OAKLAND - CALIFORNIA

TANZIA

AAleykum. 
Inna Lillah wainna ilaihi rajiuun...
Kwa niaba ya familia ya aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Na pia aliyekuwa  Mbunge wa Jimbo la Rufiji katika Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo Na pia mhadhiri katika Vyuo Vikuu Vya udaktari katika nchi mbalimbali duniani Prof.  Idris Ali Mtulia amefariki dunia Leo Jumatatu Desemba 5, 2016. 
Taratibu za msiba huo zinafanyikia nyumbani kwake Upanga, Mazengo Street jijini Dar es Salaam. 
Kwa wale ndugu Na marafiki wanaoishi hapa Marekani wanaweza kuwapa mkono wa pole Na kutoa rambirambi zao kwa watoto wa marehemu, Yusuf and Abdullah Mtulia. 
Msiba upo katika anuani ifuatayo

22637 settlers trail terrace Ashburn VA 20148
Kwa kutoa rambi rambi tafadhali tuma katika bank hii

Jina: Abdullah Mtulia
Bank: Wells Fargo
Acc#: 053000219

Tutawajulisha siku Na muda wa kufanya kisomo cha kumrehemu baba yetu Hapa DMV, Marekani

Kwa maelezo zaidi wasiliana Na 

Iddi Sandaly (301) 613-5165
Asha Nyang'anyi (301) 793-2833
Jasmine Rubama (410) 371-9966
Joha Nyang'anyi (240) 813-5563
Dr. Rukia Marijani (850) 980-6633
Shukran..

HOLIDAY MINI SESSIONS


DAS ILALA EDWARD MPOGOLO AZINDUA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJSNIA NA WATOTO WILAYANI HUMO LEO

Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akiwasili kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mwembeni, Vngunguti kwenye uzinduzi wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa Jinsia na watoto kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Mwwembeni, wilayani humo mkoani Dar es Salaam, leo. Pamoja naye ni Kamanda wa Polisi Ilala, Salum Hamdani.
Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo alifurahia jambo na Kamanda wa Polisi IlalaSalum Hamdan baada ya kuketi meza kuu

CHADEMA YAWANOA VIONGO WAKE WA MABARAZA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Lengo lilikuwa ni kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake ikiwemo kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama chadema ili kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu nchini.

Chama hicho kililaani zoezi la kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la Mwanza huku mazingira rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus alisema hatua hiyo inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa mwelekeo wa kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza machinga hao kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Na BMG Habari
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MAFINGA WILAYANI MUFINDI WAPIGWA MSASA NA POLICY FORUM

 Mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alikuwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.

na fredy mgunda,iringa


Madiwani wa halmashauri ya mji wa mafinga wilayani mufindi wameongezewa makali ya kiutendaji  na uwajibikaji na shirika lisilo la kiserikali la policy forum kutoka jiji Dar es salaam.
Akizungumza na blog hii mbunge wa jimbo la Mafinga mjini Cosato Chumi alisema kuwa mafunzo wanayopewa madiwani yanalengo la kuwaongezea uwezo wa utendaji wa kazi katika kata zao.
Aidha Chumi alisema kuwa ili kupata maendeleo ya halmashauri ya mji wa Mafinga ni lazima madiwani wawe na uelewa wa kuzishughulikia kero za wanachi na kuwa wabunifu wa kupanga mipango ya kuleta maendeleo.
“Ukiangalia madiwani wengi bado hawavijui baadhi ya vitu na kuhoji kutokana na kanuni na sheria za halmashauri hivyo nimeleta semina hii kuwaongezea uwezo madiwani wa jimbo la mafinga”.alisema Chumi
Nao baadhi ya madiwani walimshukuru mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi kwa kuwatafutia watu wa kuwapa elimu ya kiutendaji na kujua majukumu ya madiwani katika kuisimamia miradi ya halmashauri.
“Angalia tulikuwa hatujui mambo mengi na ndio chanzo tulikuwa tunamuingilia majukumu mkurugenzi kama tulikuwa tunakagua barabara za mji wa mafinga kumbe tulikuwa kinyume na utaratibu”.walisema madiwani wa mafinga
Kwa upande wake meneja uwajibikaji wa shirika lisilo la kiserikali la policy forum Richard Angelo alisema kuwa madiwani wengi wanakumbana na changamoto za kuisimamia halmashauri hivyo wameamua kuwa elimu ya kujua wajibu wao.
Hata hivyo Angelo alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa madiwani na wabunge karibia wote lengo likwa ni kukuza uelewa na uwezo wa kuongoza maeneo wanayowaongoza.
“Hivi karibu tumetoa elimu kwa wabunge mjini Dodoma na ndipo mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi alituomba tuje kutoa elimu kwa madiwani wa jimbo lake na ndio maana ndio tupo hapa mjini Mafinga”.alisema Angelo

Ungana nasi wakati tunatembelea jengo jipya la Makumbusho ya Historia ya Wamarekani Weusi hapa Washington

MFUKO WA LAPF KWA MARA NYINGINE WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UTUNZANI WA MAHESABU NCHINI

 Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa LAPF, John Kida (katikati mwenye tuzo), akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kutunukiwa tuzo ya Utunzaji Bora wa Mahesabu Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
 Mgeni rasmi katika hafla hiyo akisoma hutuba kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Profesa Isaya Jairo na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa NBAA, Pius Maneno.

WANAWAKE WAJASIRIAMALI MASOKONI WAMETAKIWA KUWA NA MSHIKAMANO

 Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Sura Mpya na Sauti Mpya Tanzania (NFNV), Emma Kawawa (kulia), akizungumza na wanawake wafanyabiashara katika masoko ya Ilala na Temeke wakati akifunga mkutano wa kupanga na kuweka mikakati ya vikundi vya umoja na umoja wa kitaifa wa wanawake (Uwawasota) kwa mwaka 2017 uliofanyika Hoteli ya  Dreamer Buguruni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika Soko la Mchikichini, Betty Mtewele (kulia), akizungumza katika ufungaji wa mkutano huo.

MWANDISHI MATHIAS CANAL ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWA KULA CHAKULA CHA JIONI NA WATOTO WA MTAANI JIJINI MWANZA

Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal mwenye shuka la kimasai shingoni akiwaelekeza watoto wa mitaani Jijini Mwanza kula kwa ufasaha pasina vurugu kama walivyozoea
 Binti Leah Mathias mtoto wa Mwandishi Mathias akiwa ameshiriki katika hafla hiyo
Mke wa Mwandishi Mathias Canal Bi Zakati Chagamba akifurahi na Mwanae Leah Mathias wakati wa hafla hiyo, Pembeni ni Teddy Fransis Mpwa wa Mathias Canal

PICHA MBALIMBALI ZA MCHEZAJI STRAIKA WA TIMU YA MBAO FC U-20, ISMAIL MRISHO HALFAN ALIYEFARIKI JIONI HII BAADA YA KUANGUKA WAKATI WA MECHI YAO KAITABA


Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc U-20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki Dunia jioni baada ya kuanguka Uwanjani Kaitaba wakati wa Mtanange wao dhidi ya timu ya vijana wa Mwadui ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la ligi ya Vijana. 
Ismail Mrisho Khalfan amefariki akiwa na miaka 19.
Ismail Mrisho Khalfan akipata huduma ya kwanza kutoka kwa madaktari wa Timu yake hii kwenye Uwanja wa Kaitaba. 

Watendaji Wanaotafuna Fedha za Miradi ya Wafadhili Mkoani Kigoma kukiona

Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machura akitoa hotuba ya kufunga mafunzo ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa washirika wa maendeleo kwa Mkoa wa kigoma. Kulia ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Dkt. Wilhelm Ngasamiaku kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kushoto ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Paul Sangawe kutoka Tume ya Mipango.
Mratibu wa Mafunzo Bw. Paul Sangawe akitoa muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika mafunzo hayo yaliyodumu kwa muda wa siku tano. Katikati ni Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Kigoma Bw. Daniel Machura na kulia ni mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Dkt Wilhelm Ngasamiaku kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

WIKI YA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA MAADILI NA HAKI ZA BINADAMU YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) akizindua rasmi Wiki ya kutoa huduma kwa wananchi katika kuadhimisha Siku ya Maadili na Haki za Binadamu inayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.