Advertisements

Tuesday, November 25, 2014

SERIKALI YAIPONGEZA TPHA KATIKA SEKTA YA AFYA NCHINI


Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando akifungua kongamano hilo la kisayansi.
Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe akitoa lecture katika kongamano hilo.


NA ANDREW CHALE, BAGAMOYO.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imepongeza juhudi za makusudi zinazofanywa na Chama cha Afya ya Jamii Tanzania (TPHA) katika kushughulikia masuala ya afya kwa jamii huku ikiahidi kushirkiana kwa ukaribu katika maboresho na kukuza juhudi za mashirika binafsi ya sekta ya afya.

Hayo yamesemwa leo Novemba 24 mjini hapa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk.
Margaret Mhando, aliyemwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando wakati wa ufunguzi wa kongamano la 31 la Kisayansi na Mkutano mkuu wa mwaka wa TPHA, katika ukumbi wa Stella Maris, Bagamoyo.

Dk. Margaret Mmbando alisema kuwa juhudi za dhati zinazofanywa na wadau sekta binafsi wa afya serikali inazitambua na watahakikisha wanaendelea kuungana nao kwa hali na mali ilikuisaidia jamaii kwenye mambo yote ya msingi hususani masuala ya afya.

"Tunaipongeza TPHA kwa juhudi hizi za dhati kabisa katka ukuaji na ustawi wa sekta ya afya. Hivyo pia naamini baada ya kongamano hili kwa muda wa siku tano kila atakayetoka hapa atajifunza mambo makubwa na ya msingi katika mustakaba wa sekta hii" alisema Dk.Margaret Mhando.

Aidha, aliwataka TPHA kutanuka zaidi kuwa na matawi mengi ikiwemo kufika pembezoni mwa nchini ilikuweza kutanua huduma zao hizo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TPHA Taifa, Dk. Elihuruma Nangawe alisema kongamano hilo la kisayansi la 31, linatarajia kuwa la siku tano na huku likitarajiwa kumalizika Novemba 28 mwaka huu ambapo wataalamu wa afya na wadau watajadilina mambo mbalimbali ya afya hapa nchini.

Naye Katibu Mtendaji wa TPHA Taifa, Dk. Oberlin Kisanga alisema kongamano hilo ni la kuwakutanisha wataalamu mbalimbali wa afya na mambo ya jamii kutoka serikalini na mshirika binafsi ambapo watajadili changamoto za ukuaji wa sekta hiyo ya afya na maboresho yake kwa pamoja sambamba na kupata ujuzi watakaofanyia kazi.

"Kongamano hili la kisayansi la 31, ambalo kwa
mwaka huutukiwa tunakutana ili kubadilishana ujuzi, uzoefu na kutoa mapendekezo namna ya kuleta mabadiliko katika jamii" alisema Dk.Kisanga.

No comments: