Advertisements

Wednesday, September 28, 2016

Sensa ya mifugo kuanza Iringa

Wilaya ya Iringa inaanza kufanya sense ya mifugo katika wilaya nzima. Zoezi hilo litaanza tarafa ya Pawaga na Idodi kuanzia tarehe 28 mwezi huu 9 na linategemea kuisha tarehe 15mwezi wa 10. Akizindua sensa hiyo katika kata ya Mboliboli tarafa ya pawaga, Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela (pichani) alisema “ kila mwenye nmifugo ya aina yoyote lazima ahakikishe inahesabiwa kwa nia moja tu ya kupanga mipango endelevu ya kilimo na ufugaji katika wilaya yetu”, alisistiza pia sensa hii itasaidia kujua takwimu halisi. Wenyeji wa kata ya Mboliboli wamepokea zoaezi hilo kwa mikono miwili na kusema hilindio suruhisho la migogoro ya wakulima na wafanyakazi.
Tarafa za Pawaga na Idodi ndio zianaongoza kwa kuwa na mifugo mingi mkoa wa iringa , pia zina changamoto kubwa ya mashamba ya wakulima kuvamiwa na mifugo. Zoezi hili litaendeshwa na watendaji wa vijiji ambapo litasaidia kupanga utaratibu mpya wa ufugaji wenye tija. “ Huu ni wakati muafaka wa kuacha kuangalia idadi ya mifugo badalayake tuangalie thamani ya mifugo tulio nayo”
Wananchi pia walitoa kero zao ikiwamo maji ambayo yanasumbua, jingo la shule kuounyesha nyufa kutokana na upepo mkali pia sula la mfereji wa umwagilaji ambao unahitaji kiasi cha shilingi bilioni 5 kurekebishwa. Akifungua Mkutano huo Mwenyekiti wa kijiji cha Migoli Mh Bosco Myombani alisema suala la mifugo ni jema sana kama tutakuwa na takwimu sahihi. Pia aliomba wadau wajitokeze kuchangia shule pamoja na miundo mbinu ya maji.

No comments: