Advertisements

Wednesday, October 26, 2016

CHAMA CHA AFYA YA JAMII (TPHA) CHAWAKUTANISHA WADAU WA AFYA KUJADILI NJIA ZA KUTUMIA KUTENGENEZA SERA YA KUPUNGUZA UNYWAJI WA POMBE

Dk. Faustine Njau kutoka Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) akifungua mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya ya Jamii ili kujadili ni kwa jinsi gani wanaweza kuunganisha nguvu katika kupinga matumizi ya pombe katika familia. (Picha na Geofrey Adroph)
Wadau wa Afya ya jamii wakiwa wamesimama kumuombea aliyekuwa Mratibu wa Mradi wa Madhara ya Tumbaku (TPHA) Dk. Bertha T.A. Maegga aliyefariki dunia.
Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii (TPHA), Dk. Mashombo Mkamba akizungumzia historia ya Chama cha Afya ya Jamii (TPHA) kwenye semina ya wadau mbalimbali wa wanaopigania matumizi ya pombe katika jamii mbalimbali hapa nchini Tanzania.

Matias Kimilo kutoka Mtandao wa kudhibiti madhara ya Pombe akizungumzia madhara yanayawakuta watoto na jamii mara baada ya familia kujikita kwenye unywaji wa pombe katika ukumbi wa NIMR  jijini Dar es Salaam leo
Judith Kimaro kutoka Manispaa ya Kinondoni akizungumzia kesi wanazozipokewa kwa siku kutokana na kuvunjika kwa ndoa ikiwa kisababishi kikubwa ni pombe
Janeth Mawinza kutoka WAJIKI akizungumzia  jinsi familia zinavyoadhiriwa na vitendo vya kijinsia vinavyosababishwa na matumizi mabaya ya pombe pamoja na nyingine kutengana kutokana na matumizi ya pombe kwa wazazi wao.
Baadhi ya wadau wa Afya wakichangia mada
Baadhi ya wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina iliyowakutanisha wadau wa Afya ya Jamii katika ukumbi wa NIMR jijini Dar es Salaam.
Loyce Gondwe kutoka TAMWA akitoa mada kuhusu sheria zinazohusu pombe kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Afya uliokutana katika ukumbi wa NIMR jijini Dar leo

No comments: