Advertisements

Monday, December 5, 2016

CHADEMA YAWANOA VIONGO WAKE WA MABARAZA WILAYA YA NYAMAGANA MKOANI MWANZA.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Lengo lilikuwa ni kuimarisha mabaraza hayo kwa ajili ya utendaji kazi wake ikiwemo kuhakikisha wanachama wapya wanaendelea kujiunga na chama chadema ili kukifanya kuendelea kuwa chama cha upinzani chenye nguvu nchini.

Chama hicho kililaani zoezi la kuwahamisha machinga kutoka katikati ya Jiji la Mwanza huku mazingira rafiki yakiwa bado hayajaandaliwa ambapo Micus alisema hatua hiyo inaweza kusababisha vijana na akina mama wengi kukosa mwelekeo wa kujitafutia kipato kwa njia sahihi ambapo walihimiza machinga hao kutengenezewa mazingira bora ya kufanyia biashara zao.
Na BMG Habari
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kanda ya Ziwa, Meshack Micus (kulia), wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Diwani wa Kaya ya Butimba, John Pambalu, akizungumza juzi kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana wakimsikiliza diwani wa Kata ya Butimba, John Pambalu, wakati akizungumza kwenye semina kwa viongozi wa Mabaraza ya Chadema Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Baadhi ya viongozi wa mabaraza ya Chadema wilayani Nyamagana, wakifuatilia kwa makini semina iliyotolewa kwa ajili ya kuimarisha uhai katika utendaji wao wa kazi ili kujiimarisha zaidi.
Viongozi mbalimbali Chadema Wilayani Nyamagana
Katibu wa Chadema Kanda ya Ziwa, Mechack Micus, akizungumza nje ya semina kwa viongozi wa mabaraza ya Chadema Wilayani Nyamagana.
John Amos, Mwenezi BAVICHA Kata ya Igoma Jijini Mwanza, akizungumza nje ya semina ambapo alipongeza semina hiyo kwamba itaendelea kukiimarisha chama.
Seko Jabanhya ambaye ni Mwenezi wa Vijana Chadema Wilaya ya Nyamagana, akizungumza baada ya semina kwa viongozi wa mabaraza Chadema wilayani Nyamagana. Alisema itasaidia chama kujiimarisha zaidi na kuendelea kuwatetea vyema wananchi.
Eather Alphaxard ambaye ni mwakilishi kutoka Kata ya Igoma ndani ya BAVICHA wilaya ya Nyamagana alisema semina hiyo itasaidia kuimarisha misingi ya viongozi wa mabaraza ndani ya chama.
Katikati ni Wilbert Mandago ambaye ni Afisa Bunge na Halmashauri Chadema akiteta jambo na viongozi wengine wa Mabaraza Chadema wilayani Nyamagana
Picha ya pamoja.

No comments: