Advertisements

Monday, December 5, 2016

MWANDISHI MATHIAS CANAL ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA KWA KULA CHAKULA CHA JIONI NA WATOTO WA MTAANI JIJINI MWANZA

Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal mwenye shuka la kimasai shingoni akiwaelekeza watoto wa mitaani Jijini Mwanza kula kwa ufasaha pasina vurugu kama walivyozoea
 Binti Leah Mathias mtoto wa Mwandishi Mathias akiwa ameshiriki katika hafla hiyo
Mke wa Mwandishi Mathias Canal Bi Zakati Chagamba akifurahi na Mwanae Leah Mathias wakati wa hafla hiyo, Pembeni ni Teddy Fransis Mpwa wa Mathias Canal

 Maelekezo ni muhimu ili kuwa na nidhamu katika kula
 Watoto wakifurahia chakula cha jioni pasina vurugu na kadhia yoyote
 Mlo unaendelea mpaka kushiba atakaye na aje
Moja wa binti aliyetelekezwa akiwa na watoto wake kushiriki mlo wa chakula cha jioni ulioandaliwa na Mwandishi Mathias Canal
 Picha ya pamoja mara baada ya kushiriki Hafla ya chakula cha jioni


Wengine ni wakubwa kabisa lakini wapo mitaani walikuwa watoto wadogo na sasa wamekua watu wazima

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mwandishi wa habari na mchambuzi wa masuala ya siasa nchini Tanzania Ndg Mathias Canal tarehe nne ya kila Mwezi wa kumi na mbili huadhimisha kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo hii leo ameadhimisha kumbukizi hiyo kwa kula chakula cha jioni na familia yake sambamba na watoto wa Mitaani (Street Children) wa JIjini Mwanza waliojitokeza kwenye hafla hiyo ya chakula cha jioni.

Canal ameamua kufanya hivyo kutokana na watoto wa mitaani hujitokeza kwa wingi kuomba msaada wa kupatiwa hela ili wanunue chakula katika eneo maarufu Jijini Mwanza la Salma Cone ndipo mwandishi huyo kwa kushirikiana na Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya METDO Tanzania walipoamua kushiriki chakula cha jioni kwa kula na watoto hao.

Akizungumzia maamuzi hayo ya kukacha kwenda Beach ama maeneo ya kuvinjari kama ambavyo waadhimishaji wengine hufanya Mathias Canal alisema kuwa ni jambo la thawabu sana kwa Mungu na kwenye jamii kwa ujumla kushiriki chakula cha jioni na watotot wa mitaani kwani asilimia kubwa wapo katika mazingira ya kuomba kutokana na hali ngumu za maisha zinazozikabili familia zao, lakini pia wapo watoto wengine ambao walitelekezwa na wazazi wao jambo ambalo limesababisha kuwa katika maeneo yasiyo rasmi na kujihusisha na tabia ovu.

”Serikali inapaswa kuwa na mkakati mathubuti wa kuwasaidia watoto hawa kwani kuwaacha waendelee kuwa mitaani ni njia mojawapo ya kuzalisha Wezi na Majambazi, Malaya na Mashoga hii ni kutokana na vitendo ovu wanavyofanyiana wenyewe kwa wenyewe watoto hawa au kufanyiwa na watu wengine kwa kubakwa na kulawitiwa” Alisema Canal

Serikali kupitia wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapaswa kulitaza jambo hili kwa umakini  kwani Tanzania inaendelea kuwa na watoto wengi wa mitaani hususani katika majiji na maeneo ya mikoa mbalimbali ili kunusuru Taifa lenye vijana wengi wa badae wasiokuwa na elimu na hatari kwa wananchi wengine kuna kila sababu ya kuweka mikakati ya kukabiliana na kadhia hiyo.

Kuna taarifa kuwa idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi nchini imezidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha. Hii inatokana na idadi hiyo kufikia watoto 897,913, ambao wote wamekuwa wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha inayoambatana na vitendo vya ukatili kila uchao.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka jana zinazoonyesha kuwa watoto milioni 2.5 wamekuwa yatima baada ya wazazi wao kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ukimwi na wakati huohuo, watoto wa kike watatu kati ya 10 wamebainika kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18.

Hakika, idadi hii ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu inatisha. Sisi tunaona kwamba sasa kuna kila sababu kwa serikali na jamii nzima kutafuta namna bora ya kuwasaidia watoto hawa kwani vinginevyo, athari zake zinaweza kuwa kubwa kwa taifa kuliko inavyoweza kudhaniwa.

"Maisha ya mjini ni magumu sana. Mtu kulala nje, kwenye baridi na mara nyingine unanyeshewa mvua. Kuna wakati unaweza kuamka asubuhi na kukuta mwenzenu amekufa," Anasema mmoja ya watoto hao, msichana mwenye umri wa miaka 16, anasema wengine huishia kuuza miili yao ili kupata fedha za kununua chakula kabla ya kuanza kutafakari namna ya mahala pa kulala na usalama wao kimwili na kiakili.

Naye Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye usajiri No. ooNGO/08317 inayojishughulisha na kutoa Elimu ya Mazingira kwa wananchi wanaozunguka migodi pamoja na wafanyakazi wa migodini Bw Ashraf Omary  amekiri kuwa  athari za kuwapo kwa watoto wanaoshi katika mazingira hatarishi ni kubwa kwa taifa na hivyo, wakati jitihada za kukabiliana na visababishi vya kuwapo kwa watoto hao zikiendelea kufanywa, upo ulazima pia wa kuhakikisha kwamba watoto hawa waliopo mitaani wanapatiwa upendo na huduma zote kama ilivyo watoto wengine.

”Ikumbukwe kuwa, ikiwa watoto wa mitaani wataendelea kuachwa wajitafutie wenyewe maisha yao, ni dhahiri kwamba nao hawatakuwa na upendo kwa jamii inayowazunguka pindi watakapokuwa watu wazima na hatimaye kuishia kuwa wakabaji pasina kuwa na huruma maana hawakupata upendo na huruma kwa jamii wangali wadogo” Alisisitiza Ashraf Omary

Akizungumza na watoto hao mara baada ya kumaliza kula chakula cha jioni Mathias Canal alisema kuwa Katika kukabiliana na swala hili ni muhimu serikali kukabiliana na changamoto ya umasikini uliokithiri nchini Tanzania ndio njia pekee ya kunususru Taifa kuwa na tegemezi wengi tena wenye chuki na hasira na jamii yao kwa kukosekana upendo wa dhati.

MWISHO

1 comment:

Anonymous said...

Jeustawi wa jamii Bongo wana mipango gani kuwasaidia hawa watoto wa mitaani? Tusishangae baathi yao kuwa majambazi sugu miaka michache ijayo na kuhatarisha maisha yetu wote...something needs to be done NOW...Rais Magufuli tusaidie...ili nalo ni JIPU SUGU!

~CK-USA