Advertisements

Friday, April 28, 2017

KIKOSI KAZI CHA KUNUSURU MTO RUAHA CHATOZA FAINI MASHAMBA YA MPUNGA NA SKIMU ZA UMWAGILIAJI WILAYANI MBALARI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA .

Mashamba ya mpunga ya Mbarali Highland Estates, Kapunga Rice Project, Kapunga Small Holders farm, pamoja na skimu za umwagiliaji za Mwanavala (Nguvukazi farm), Mwashikamile pamoja na Sikimu ya Mwendamtitu zilizoko Mbarali mkoa wa Mbeya yametozwa faini ya jumla ya kiasi cha shilingi 120,290,000/= baada ya kukiuka sheria mbalimbali za Mazingira zilizo chini ya Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Faini hiyo inayotakiwa kulipwa ndani ya siku kumi na nne kuanzia tarehe 27 aprili 2017, imetozwa na Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kuokoa Ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kilichoko Mkoani Mbeya kupitia kwa Mwananasheria wa NEMC- Vicent Haule , baada ya kugundua makosa mbalimbali ya uvunjifu wa sheria za mazingira na umwagiliaji katika Mashamba hayo wakati wa ziara ya kutembelea mashamba ya Mpunga na skimu tofauti za umwagiliaji wilayani humo.

Akiongea na Waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Kikosi kazi hiko cha Kitaifa Bwana Richard Muyungi, alisema kwamba kutokana na makosa mbalimbali yaliyokutwa katika masahamba hayo ikiwemo kutokuwa na vyeti vya ukaguzi wa Mazingira, kukiuka taratibu za umwagiliaji kwa kutoa na kutumia maji bila ruhusa, kuweka mifereji mikubwa ya kumwagilia mashambani pasipo kufuata sheria na kanuni zinazotakiwa, kutorekebisha miundombinu ya Umwagiliaji kwa mifereji ya kutolea maji. Mashamaba hayo yanapigwa faini kama ifuatavyo Mbarali Estates 33,000,000, Kapunga Rice Project 33,100,000/=, Kapunga Small Holders 3,000,000/=, Madibila farm Project 33,000,000. Pamoja na mashamba hayo pia zipo skimu za Umwagiliaji zilizotozwa faini ikiwepo Skimu ya Mwendamtitu 7,995,000, Mwanavala (Nguvukazi) 7,995,000/=, Mwashikamile 2,200,000/=.

Aidha aliongeza pia mashamba ya Mwashikamile, Mwanavala(nguvu kazi) na Kapunga Small Holders, wanatakiwa kulipa faini lakini pia baada ya kuvuna wanatakiwa kuacha mara moja kulima tena katika mashamba hayo mpaka pale watapofuata taratibu za kupata vibali vya maji na cheti cha ukaguzi wa mazingira kutoka NEMC na Mamlaka ya Bonde la Mto Rufiji ."Kutoza faini hizi siyo kukomoa Mashamba haya ila ni kuhakikisha kuwa Wamiliki wa mashamaba makubwa ya umawagiliaji wote Nchini wanafuata taratibu na Sheria za kimazingira katika kuendesha mashamba haya" alisema Muyungi

Kikosi kazi hiko kiko MKoani Mbeya kwa kukagua na kutembelea sehemu mbalimbali za mashamba , skimu za umwagiliaji na pia kusikiliza maoni ya Wananchi jinsi ikiwa ni harakati za kurudisha ikolojia ya mto Ruaha.

No comments: