Advertisements

Saturday, August 19, 2017

UVCCM YASIFU UTEKELEZWAJI WA ILANI YA UCHAGUZI PEMBA

  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza na kikundi cha wajasiliamali  kikundi cha ushoni Mchanga mdogo Mkoa wa Kaskazini pemba wilaya  Wete.
 Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(wa kwanza kushoto) akishiriki ujenzi wa Jengo la maskani Mtambwe Wilayani wete.

 wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili  kuzungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
  Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakifuatilia kwa Umakini mkutano huo.
   Kaimu katibu  wa Idara ya Uchumi Uwezeshaji na Fedha (UVCCM) ndg:Dorice Obed akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Pemba Khadija Nassoro Ally akizungumza katika Mkutano wa ndani  akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano wa ndani akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Wanachama na Viongozi wa CCM na Jumuiya zake Wilaya ya Wete wakimsikiliza
  Kaimu katibu mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka(PICHA ZOTE NA FAHADI SIRAJI)
....................................................................................................................................................................

Na Mathias Canal, Kaskazini Pemba

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Umeipongeza serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Visiwani Pemba.

UVCCM imesema kuwa RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein amefanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ikiwemo kuundwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya ndege vya Zanzibar jambo ambalo litaongeza mapato kwa serikali na vipato kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Ndg Shaka Hamdu Shaka leo Agosti 17, 2017 alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya muundo wa Umoja wa Kitaifa (SKU) imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha uongozi wa miaka saba cha Dkt Shein.
Alisema kuwa kuwepo kwa Serikali hiyo kumeweza kuleta  maelewano ya kisiasa pamoja na kuvishirikisha vyama vingine katika uwezeshaji wa serikali.
Alisema kuwa sekta ya elimu imeimarika kwa kiasi kikubwa jambo ambalo linazidi kurahisisha upatikanaji wa elimu bora ikiwemo kuimarika kwa mishahara ya wafanyakazi Visiwani Zanzibar.

Alisema kuwa uvumilivu wa kisiasa na kuheshimu Katiba na sheria ndio siri ya mafanikio ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwemo kuheshimu katiba, utawala bora, kupinga udhalilishaji kwa watoto na wanawake.

Awali akizungumza na vijana wa Maskani ya Subira yavuta kheri iliyopo eneo la Mgogoni, Shaka alisema kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF aliyesimamishwa uongozi Maalim Seif Shariff  Hamad anapaswa kupumzika na kuacha siasa za kuwagawa wananchi badala yake amemtaka awe kuungo katika kujenga umoja na mahusiano.

Shaka yupo ziarani Kisiwani Pemba ambapo atatembelea mikoa yote miwili ya Kusini Pemba na Kaskazini Pemba ambapo pia atazuru katika Wilaya zote nne ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Wete, Micheweni, Mkoani na Chakechake kwa kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

MWISHO.

No comments: