Advertisements

Thursday, December 7, 2017

Ecobank Tanzania yasaidia kupatikana kwa maji safi kwa Shule ya Hananasif


Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee – kulia, akimkabidhi vitabu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hananasifu Idda Uisso iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akijaribu moja ya mifereji ya maji salama katika wa Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.


Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Mwanahiba Mzee akikata utepe kuashiria upatikanaji wa maji Shule ya Msingi Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule hiyo ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso..
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Hananasifu Idda Uisso akimwonyesha Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank baadhi ya mifereji ambayo kwa sasa inatoa maji salama baadhi ya kufanyiwa ukarabati na benki hiyo.
Mmoja wa mfanyakazi wa Ecobank akinawa kuashiria kuanza kupatikana kwa maji salama baada benki hiyo kutengeneza miundombinu na kusafisha mifereji iliyokuwa imeziba katika shule ya Msingi ya Hananasifu iliyopo wilaya ya Kinondoni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Ecobank wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso.
Diwani wa Kata ya Hananasifu akitoa neon la shukrani kwa uongozi wa Ecobank Tanzania. Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo kwenye shule ya Msingi Hananasifu, Kinondoni ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Ecobank. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idda Uisso. 
Ecobank Tanzania Ltd imesaidia uwekaji wa miundombinu bora pamoja na tanki maalum ili kurahisisha usambazaji pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika vyoo na maeneo yenye uhitaji wa maji kwa wanafunzi na waalimu wote wa shule ya Msingi ya Hananasif iliyopo katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya Ecobank ambayo hufanyika kila mwaka katika nchi 33 barani Afrika ambapo Ecobank inafanya biashara.

Msaada huo wa Ecobank Tanzania kusaidia shule hiyo kupata maji safi umetolewa leo ikiwa njia moja wapo ya kuadhimisha kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Ecobank inayosema ‘Maji Salama, Ishi na Afya njema’ Safe Water, Healthy Living’

Mbali na Ecobaank kutoa msaada huo, wafanyakazi wa Ecobank Tanzania pia wamejumuika kwenye kufanya usafi wa mazingira shuleni hapo kwa kuzibua mitaro ya maji taka yote pamoja na kuweka dawa kwenye kisima cha maji shuleni hapo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata maji safi na salama.

Kwa upande wa elimu, Ecobank pia imetoa vitabu kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na kutoa tuzo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi kwenye mitihani yao kuanzia darasa la kwanza hadi la sita.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Bi Mwanahiba Mzee alisema benki hiyo imekuwa ikiadhimisha siku ya Ecobank kwa kutoa sehemu ya faida wanayopata kwa Jamii inayowazunguka.

“Tuliguswa sana baada ya kupewa taarifa kuwa shule ya Hananasif ina jumla ya wanafunzi 728 lakini miundombinu ya maji imeziba na kubakia na sehemu moja tu ambayo inatumiwa na shule nzima. Vyoo havina maji na hivyo imekuwa ni changamoto ya kiafya kwa wanafunzi, walimu na watu wengine kwenye shule hii, tukaona ni vyema kuja kusaidia ” alieleza Mwanahiba Mzee 

Bi Mzee, alisema kutokana na Benki yake kutoa msaada huo, pamoja na vitabu vya kiada, motisha yaa zawadi kwa wanafunzi itasaidia kutoa hamasa kwa wanafunzi kuendelea kuongeza bidii kwenye masomo yao zaidi

“Ecobank Tanzania inatambua umuhimu wa kuwa na miundombinu bora pamoja na kuboresha elimu ikiwa ni dhamira yetu katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuinua kiwango cha elimu hapa nchini, aliongeza Bi Mwanahiba Mzee .

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Hananasif Mwalimu Idda Uisso Alitoa shukrani kwa juhudi za Ecobank Tanzania kwa kuhakikisha shule hiyo inapata maji salama. “Nachukua hii fursa kuwapongeza uongozi wa Ecobank Tanzania kuchagua kuja shule ya Hananasif kwani hapa kuna shule zingine nyingi.

Alisema changamoto kubwa ilikuwa ni maji kwani kwa Idadi kubwa ya wanafunzi walionao maji safi na salama ni muhimu. “Kwa msaada wa mamboresho ya miundombinu yote mliyofanya, kwa sasa tuna uhakika wa maji safi na salama kwa waalimu pamoja na wanafunzi” alisema.

Vile vile alitoa shukrani za dhati kwa msaada wa vitabu pamoja na zawadi kwa wanafunzi bora kwani kutaongeza hamasa kwa wanafunzi. “Sisi kama shule tumekuwa tukifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa lakini kwa msaada wa vitabu na kuhamasisha wanafunzi, nina uhakika na ninawaahidi Ecobank tutaendelea kufanya vizuri zaidi”.

Ecobank sasa inafakisha miaka 8 hapa nchini Tanzania huku ikiwa na matawi ya kutoa huduma bora za kibenki katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha

No comments: