Advertisements

Tuesday, February 13, 2018

MSHINDI WA TATU MZUKA AWAANDALIA CHAKULA CHA PAMOJA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

Mshindi wa mchezo wa kubahatish wa Tatu Mzuka aitwaye Mrisho Maganga aliyejinyakulia kitita cha shilingi Milioni 22, hivi karibuni amefanikiwa kufanya Dua ya kumshukuru Mungu  pamoja na Watoto wa kituo cha Watoto yatima cha Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni.Maganga alisema kuwa aliamua  kufanya Dua pamoja na kula chakula cha pamoja na watoto hao ikiwa ni sehemu ya kumshukuru Mungu kwa kila jambo.Alisema mara baada ya kufanikiwa kuzipata zile fedha ameziingiza kwenye miradi yake aliyokwa ameipanga kuifanya muda mrefu.
Pichani kushoto ni Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka Patronela Nicolaus akiwa pamoja na baadhi ya wadau wa Kituo hicho cha Watoto waishio katika mazingira magumu, Umra Orphanage Center kilichopo Magomeni

No comments: