Advertisements

Tuesday, April 24, 2018

NIMERIDHISHWA NA MAADHALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO-MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama onesho lahalaiki, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera na Uratibu) Profesa Faustine Kamuzola, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu , Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr Florens Turuka, naMkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja  wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwapungia  wananchi, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki  ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.

“Nimeridhika na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.”

Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.

No comments: