Advertisements

Tuesday, April 24, 2018

PUMA ENERGY TANZANIA YAZINDUA MAFUNZO MAALUM YA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI

Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti akizungumza kuhusu wanavoshiriki na kufanikisha mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi hapa nchini ambapo kwa mwaka huu watatoa mafunzo kwa shule 22 kwa mkoa wa Ruvuma na Dar es Salaam.
Trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu akinzumgumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoa ya Dar es Salaam.
 Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend, Simon Kalolo akizungumzia mafunzo ya usalama barabarani wanayoyatoa kwa wanafunzi wa shule za msingi wakati wa uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo uliofanyika Makao makuu ya Kampuni ya Puma leo jijini Dar es Saaam.
 Mshindi wa mchoro 2017, mwanafunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Mbande, Nasri Mustafa akiwaonyesha  mchoro wake wa usalama barabarani alioshindawakati wa uzinduzi wa mafunzo ya Usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kutoka kulia, Meneja Miradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend, Simon Kalolo, meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu na Sajent Hussein Ramadhani. Picha na Emmanuele Massaka,Globu ya jamii

 Walimu na wanafunzi pamoja wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar as Salaam.

 Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, Trafki kutoka makao makuu, ASP Mbuja Matibu wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo uliofanyika Makao makuu ya Kampuni ya Puma leo jijini Dar es Saaam.


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

KAMPUNI ya Puma Energy Tanzania imezindua kampeni maalumu ya mafunzo ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa shule za msingi kwa lengo la kueneza elimu hiyo kuanzia ngazi ya chini. 

Kampeni hiyo inayokwenda sambamba na mashindano ya uchoraji michoro ya usalama barabarani imezinduliwa Dar es Salaam jana na ofisa wa Polisi, ASP Mbuya Matibu, kutoka Makao Makuu ya Kikosi cha Usala,ma Barabarani.


AKizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo, ASP Matibu,  alisema Puma Energy Tanzania, wana mchango mkubwa katika utoaji elimu ya usalama barabarani, hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.


Pia, aliwataka madereva nchini wasiendeshe magari kwa kukariri sheria,  bali wazitambue ili waweze kuzitumia vizuri kupunguza ajali.


Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema elimu ya usalama kwa wanafunzi ni muhimu, kwani inawapa uelewa wa matumizi ya barabara kwa usalama.


"Tunawaangalia sana watoto wa shule za msingi kwani wao wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani," alisema Corsaletti na kuongeza;


"Hivyo kwa kuwafundisha usalama barabarani tunawapa ufahamu wa kuwajenga katika matumizi salama ya barabara...hiki ndicho kipaumbele chetu."


Alifafanua kwamba baada ya mafunzo  wanafunzi wanapewa nafasi ya kuchora michoro ya usalama barabarani na mshindi pamoja na shule anayotoka wanazawadiwa.


Corsaletti alisema kampuni hiyo ilianzisha mafunzo hayo mwaka 2013 na imeendelea kufanya hivyo hadi sasa kwa kufikia shule 47 na kuwafundisha wanafunzi 60,000 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro na Geita.


Aliongeza kuwa uchunguzi uliofanywa umeonesha kuwa kiwango cha ajali katika shule zilizopatiwa mafunzo kimepungua.



Corsaletti, alisema kampuni hiyo itaendelea na kampeni ya usalama barabarani na kuahidi kufanyakazi pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani, maofisa kutoka manispaa au wilaya zinakotoka shule  zilizochaguliwa ili kuhakikisha lengo linatimia.

No comments: